Rais Dkt Magufuli azindua Rasmi kiwanda cha Bakhresa
Rais Dkt Magufuli azindua rasmi kiwanda cha Bakhresa cha kuchakata matunda kilichopo Mwandege mkoni wa Pwani.
Tanzania ni ya pili kwa ukuaji wa uchumi, lakini vyombo vya habari hutasikia vikizungumzia- Rais @MagufuliJP
Ukificha fedha ardhini zitaharibika, lakini ukijenga kiwanda kitawasaidia watanzania wote- Rais@MagufuliJP
Mtu hata kama ulipata fedha zako kivyovyote, nenda ukajenge kiwanda uache kuzificha ardhini- Rais@MagufuliJP
Na ile sukari niliyoishikilia bandarini, leo Waziri wa Viwanda uhakikishe inaachiwa- Rais @MagufuliJP
Tunataka Watanzania 40% wapate ajira kutoka katika sekta ya viwanda- Rais@MagufuliJP
Kwa sasa, sekta ya viwanda inachangia pato la taifa 7.3% na sisi tunata ifike 15%- Rais@MagufuliJP
Nitoe wito waliohodhi mashamba, nitayafuta niwape wawekezaj wenye nia nzuri- Rais @MagufuliJP
Ukiona hilo eneo halikutoshi baada ya kujenga kiwanda, njoo nitakuongezea shamba lingine- Rais @MagufuliJP
Baada ya siku 5, Waziri wa Viwanda ataenda kukuonyesha hilo eneo, ulime miwa uzalishe sukari- Rais @MagufuliJP
Kama utakubali Bakhresa, mimi naweza kukupa shamba bure ulime miwa na kuzalisha sukari yako- Rais@MagufuliJP
Hii ni kutokana na baadhi kuagiza sukari ya viwanda lakini inauzwa kwa matumizi ya nyumbani- Rais@MagufuliJP
Umezungumzia gharama za sukari ya viwandani, na mimi najua kuna yako nimeizuia bandarini- Rais@MagufuliJP
Tutajadiliana hili na OMR kuona tunachoweza kufanya sababu tunaelewa hoja mlizozitoa (2/2)- Rais @MagufuliJP
Mmesema mnatumia mifuko ya plastic kuhifadhi bidhaa na sisi tunataka kuzuia matumizi (1/2) - Rais @MagufuliJP
Kama urasimu unakuwa mkubwa, tunaweza kujenga 'One stop center' kwa ajili ya wafanyabiashara- Rais@MagufuliJP
Kuhusu ombi la kutumia gesi asilia, Wizara ya Nishati na Viwanda zitajadilia juu ya hili- Rais @MagufuliJP
Ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika kiwandani kama mnataka kazi yenu- Rais @MagufuliJP
Sisi tunataka viwanda, wao wanashindwa kuleta umeme wanatukwamisha, haiwezekani- Rais @MagufuliJP
Nilichaguliwa kushughulikia mashetani na hili la TANESCO nitaanza nalo- Rais @MagufuliJP
Hatuwezi kuwa tumekaa mtu anatumia jenereta, gharama zinaongezeka na TANESCO mpo tu- Rais @MagufuliJP
Leo ni tarehe 6, wafanyakazi wa TANESCO kama mnataka kazi, kabla ya Disemba umeme uwe umefika- Rais @MagufuliJP
Umesema kuna tatizo umeme hautoshi, hawa wafanyakazi wa TANESCO Pwani na wapo wapi?- Rais @MagufuliJP
Serikali ninayoiongoza mimi itashirikiana na ninyi bega wa bega- Rais @MagufuliJP
Huu ni mwanzo mzuri kwani mazao ya wakulima hayatakuwa yakiharibika tena- Rais@MagufuliJP
Nimefurahi kuona bidhaa zako zinatengenezwa na matunda yanayolimwa nchini- Rais@MagufuliJP
Ukitembea nchi nzima, utajionea umetengeneza ajira za watu wangapi, hadi kule chato wapo- Rais @MagufuliJP
Bakhresa ni mzalendo wa kweli, mimi ni mgumu kukubali, lakini kwako nimeani, tembea kifua mbele- Rais @MagufuliJP
Tangu nichaguliwe kuwa Rais, hiki ni kiwanda changu cha kwanza kufungua, nafurahi sana- Rais@MagufuliJP